Sunday, November 1, 2015

ASILI YA WAKAGULU

Wakagulu ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa MorogoroWilaya ya Kilosa. Lugha yao ni Kikagulu... wakagulu ni mojawapo ya makabila makubwa katika mkoa wa Morogoro, wakagulu zaidi wapo katika wilaya za Kilosa, Gairo, Mpwapwa, Kongwa, Kiteto na sasa wanatanuka zaidi maeneo ya handeni. Ukifuatilia Simulizi za wazee, hususani wakati wa sherehe za kumaliza msiba (mwidiki) inaonesha kuwa wakagulu walitokea maeneo ya Rwanda na Burundi (ya sasa). Walitoka meaneo hayo kutokana na ukame uliokuwepo na matatizo mengine ya kivita. Walipita maeneo mengi yakiwemo KONONGO(UKIMBU)., Mkoani Rukwa baadae walipita maeneo ya Mkoa wa Singida hadi wakaingia RUDI (KUSINI MWA MPWAPWA). Baada ya kuishi hapo kwa muda waliparamia milima ya Rubeho, lakini bado walikuwa na mawasiliano makubwa na watu wa Konongo. Katika kuzunguuka hapa na pale huko milimani ndipo zilipojitokeza Koo mbalimbali za wakagulu kutokana na matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiwapata wanawake. Kwa msingi huo wakagulu wanachukua ukoo ( welekwa )kutoka kwa mama. Kwa mfano ukoo wa Wambigo ulipatikana baada ya wahenga kukanyaga maji yaliyokuwa yanajizunguusha (Gakubiga) kwenye mto Mkondoa.

No comments:

Post a Comment