Sunday, March 29, 2015

KATIBA YA KIKUNDI CHA WAKULU WA UKAYA (WAWAU)


TOLEO LA KWANZA
S.L.P 92 IMEANDALIWA
Mahali - Gairo AGOSTI, 2014.



KATIBA YA KIKUNDI CHA WAKULU WA UKAYA SEHEMU YA KWANZA

TAARIFA ZA KIKUNDI

1.1. JINA LA KIKUNDI.
UMOJA WA WAKULU WA UKAYA Maana ya “Wakulu wa Ukaya” ni watu wazima wenye hekima wa nyumbani/au wanaotoka katika jamii fulani.

1.2. MAKAO MAKUU YA KIKUNDI
Makao makuu ya kikundi yatakuwa Gairo ila yanaweza kubadilika pale inapobidi.
1.3. ANUANI YA UMOJA NA MAHALI
Kwa sasa anuani ya kikundi itakuwa ni:-
Jina la Kikundi UMOJA WA WAKULU WA UKAYA
S.L.P- 92 Mahali – Kisimani - Gairo

1.4. ENEO LA SHUGHULI ZA KIKUNDI
Kikundi hiki kitaendesha shughuli zake kwenye wilaya ya Gairo, na pale inapobidi kikundi kinaweza kupanua shughuli zake na kuifikia wilaya zingine.

1.5. WALENGWA NA WANUFAIKA WA KIKUNDI
Walengwa wa kikundi au umoja huu ni watu wote wenye asili/wazawa wa ukanda wa ukagulu ambao watakuwa tayari kujiunga na kikundi kwa kukubaliana na masharti na kanuni za kikundi hiki pamoja na katiba yake.Pamoja na kuwa tayari kujishughulisha na maendeleo ya Gairo katika nyanja za afya,elimu,utamaduni na uchumi.

1.6. NEMBO NA MUHURI WA KIKUNDI
Kikundi kitakuwa na nembo ambayo ni mduara wenye mlima, moto na watu ndani yake ambao wanalima kwa pamoja.

SEHEMU YA PILI

MALENGO YA KIKUNDI
2.1 DIRA NA DHAMIRA KUU

DIRA
Kuwa na umoja thabiti na imara wa wakazi wote Gairo wa ndani na nje ya nchi wanaopendana, shirikiana na kushiriki kikamilifu kuinua ukagulu kujiletea maendeleo katika nyanja zote za maendeleo endelevu ya Kiuchumi, Kielimu, Kiafya na Kiutamaduni.

DHAMIRA KUU
Kuhakikisha kuwa umoja thabiti na imara ili kujenga jamii ya wakagulu wanaopendana, shirikiana na kushiriki katika nyanja zote za maendeleo endelevu ya Kiuchumi, Kielimu, Kiafya na Kiutamaduni.

2.2 MADHUMUNI YA KIKUNDI
2
Kikundi cha UMOJA WA WAKULU WA UKAYA kitakuwa na madhumuni ya msingi yafuatayo:-
I. Kuongeza ari na hamasa ya wanakikundi na jamii kupiga vita umaskini wa kipato na ukosefu wa chakula.
II. Kusaidiana wakati wa sherehe,majanga na vifo.
III. Kusaidia na kuwezesha wanakikundi na jamii katika kuzitambua na kuzitumia kikamilifu fursa za kujiendeleza kupitia kilimo cha mahindi, maharage, viazi na mazao mengineyo.
IV. Kusaidia jamii kupata stadi na mbinu bora za kilimo, usindikaji kuongeza ubora wa mazao, na upatikanaji wa pembejeo ili kuinua uzalishaji wa mazao.
V. Kuwezesha wanakikundi na jamii kiujumla kupata stadi na mbinu za kuwa wenyeji/wazawa mahiri.
VI. Kusaidia wanakikundi na jamii kwa ujumla katika kutafuta na kujiunga na masoko ya kuaminika ya bidhaa zinazozalishwa katika kilimo.
VII. Kuchochea michezo kama njia ya kujenga umoja na mshikamano.

SEHEMU YA TATU

UANACHAMA KATIKA KIKUNDI

3.1 SIFA ZA WANACHAMA WA KIKUNDI
Uanachama katika kikundi cha UMOJA WA WAKULU WA UKAYA ni kwa kila mtu ambaye ni raia wa Tanzania, mwenye akili timamu, mwenye utayari na aliye na mtazamo wa kujisaidia na kujiwezesha pamoja na kuwawezesha wengine kujiletea maendeleo endelevu katika nyanja za Kilimo, Kibiashara na Kiuchumi kwa ujumla. Kila mwanachama ni sharti awe amesoma Katiba hii na kuielewa vyema na kukubaliana na masharti, taratibu, kanuni na maelekezo yaliyomo katika katiba hii na kuilinda bila haya.

3.2 AINA ZA WANACHAMA WA KIKUNDI
Kikundi cha WAKULU WA UKAYA kitakuwa na wanachama wa aina moja tu ambao ni:-
i. Uanachama wa mtu mmoja mmoja mwenye ari ya kujituma na kujitolea na hamasa ya kujiwezesha pamoja na kuwawezesha wengine kupata maendeleo.

3.3 NAMNA YA KUJIUNGA UANACHAMA WA KIKUNDI
Mtu anayehitaji kujiunga na unachama katika kikundi cha UMOJA WA WAKULU WA UKAYA atapaswa kuandika barua kwa Kamati ya Utendaji kuomba kujiunga au kujaza fomu ya kukubali kujiunga na kikundi. Kikundi kitajadili na kumjulisha muombaji kuhusu maamuzi yaliyofikiwa.

3.4 HAKI ZA MWANAKIKUNDI
Kwa mujibu wa Katiba hii kila mwanakikundi atakuwa na haki za msingi kama zifuatavyo:-
I. Kuwasiliana na uongozi/viongozi na kupokea taarifa za kikundi.
II. Kuhudhuria na kuwakilishwa katika mikutano/vikao tofauti.
III. Kuchagua na/au kuchaguliwa kuwa kiongozi wa kikundi. Mwombaji yeyote wa uongozi atapaswa kujaza fomu ya kuomba nafasi ya uongozi.
IV. Kupiga kura moja katika kila uchaguzi.
V. Kujieleza na kujitetea katika kikundi.
3
VI. Kujengewa uwezo na kikundi kutokana na shughuli mbalimbali kama vile mafunzo na huduma nyinginezo zinazotolewa na kikundi kwa ajili ya maendeleo ya wanakikundi.
VII. Kutumia mali za kikundi kwa kufuata utaratibu uliopo.

3.5 WAJIBU WA MWANAKIKUNDI
Kila mwanakikundi atakuwa na wajibu wa msingi katika kikundi cha Wakulu wa Ukaya ni kama ifuatavyo:-
i. Kuhudhuria vikao na mikutano mbalimbali ya kikundi.
ii. Kulipa ada na michango mbalimbali ya kikundi.
iii. Kushiriki katika utekelezaji shughuli na mipango ya kuimarisha na kuendeleza kikundi.
iv. Kujitoa na kujitolea kwa ajili ya ufanisi na maendeleo ya kikundi.
v. Kuheshimu na kutoa ushirikiano unaohitajika kwa uongozi/viongozi waliopo madarakani kwa manufaa ya kikundi.
vi. Kutafuta habari na taarifa muhimu zitakazosaidia kuimarisha na kuendeleza kikundi.

3.6 KUKOMA UANACHAMA KATIKA KIKUNDI
Uanachama wa kikundi unaweza kukoma kwa msukumo wa kikundi au mwanakikundi mwenyewe. Mwanakikundi anapoamua kukomesha uanachama wake atawajibika kulipa madeni yake kwa kikundi kabla ya kukubaliwa kujitoa kwenye kikundi. Mwanakikundi anaweza kukoma uanachama ikiwa yatatokea miongoni mwa mambo yafuatayo:-
I. Mwanakikundi kuacha kwa hiyari yake mwenyewe Mwanakikundi atapaswa kutoa taarifa ya maandishi ya mwezi mmoja na kurudisha mali zote za kikundi.
II. Mwanakikundi kushindwa kulipa ada ya mwaka kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo.
III. Mwanakikundi kwenda kinyume na maadili ya kikatiba ya kikundi, kikundi kitamwondoa kwa maamuzi ya uongozi wa juu.
IV. Mtu akifariki au kikundi kikisambaratika
V. Mwanakikundi itakapobainika na kuthibitika ametumia jina la kikundi/mali za kikundi kisiasa au kwa namna yoyote kukihusisha kikundi katika siasa au mambo yake binafsi yasio na maslahi na mlengo wa kikundi.
VI. Ikitokea mwanakikundi yeyote atafariki basi watarudishiwa ada na hisa zake kwa wategemezi.
VII. Mwanakikundi kutohudhuria mikutano mikuu ya kikundi kwa mara tatu mfululizo bila taarifa.
Endapo mwanakikundi atakoma uanachama kwa sababu zilizoorodheshwa hapo juu, hatarudishiwa kiingilio, ada na hakuna haki ya kudai au kupewa mali yoyote, isipokuwa tu mwanachama amefariki na hakuwa nadeni kwenye kikundi.

SEHEMU YA NNE
UONGOZI, UENDESHAJI NA USIMAMIZI WA KIKUNDI

4.1 MUUNDO WA KIKUNDI
Muundo wa kikundi cha WAKULU WA UKAYAutakuwa ni kama ifuatavyo:-

MKUTANO MKUU

4.2 KAMATI ZA KIKUNDI
Kikundi kitakuwa na kamati nne muhimu ambazo zitasaidia uendeshaji na usimamizi wa shughuli za kikundi. Kamati hizo ni:
  • Kamati tendaji.
  • Kamati ya Mipango na fedha.
  • Kamati ya Uzalishaji na
  • Kamati ya Masoko.

4.2.1 KAMATI TENDAJI YA KIKUNDI
Kamati tendaji ya kikundi ndiyo msimamizi mkuu wa kila siku wa masuala yote ya kikundi. Kamati tendaji itaundwa na watu saba ambao ni mwenyekiti, katibu, mweka hazina, mratibu wa uzalishaji na mratibu wa masoko na wanachama wawili watakaowakilisha wanachama wengine.Majukumu ya kamati tendaji yatakuwa ni:
i. Kuandaa Kanuni, Sheria na Taratibu mbalimbali vitakavyotumika kuendesha kikundi na kuwasilisha kwa wanakikundi kwa majadiliano na makubaliano. Kanuni yoyote haitakubalika na kikundi isipouwa pale tu itakapopitishwa na wanachama kwenye mkutano mkuu.
ii. Kusimamia shughuli za kila siku za kikundi.
iii. Kuandaa, Kuratibu, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Mipango,
Programu na/au Shughuli zinazofanywa na kikundi.
iv. Kufanya tathmini ya kiuwezo kwa kamati za Uzalishaji, masoko
pamoja na Mipango na fedha na kupima uendeshaji na maendeleo ya kikundi kila baada ya miezi mitatu (3).
v. Kutoa taarifa za tathmini za kiuwezo wa kikundi na kutoa ushauri na
mapendekezo kwa Kamati husika na wanakikundi juu ya mwenendo wa kikundi kiujumla.
vi. Kuandaa taarifa za utendaji, utekelezaji na maendeleo ya kikundi na
kuwasilisha kwa wanakikundi kwenye mkutano mkuu wa kikundi.

MWENYEKITI

KAMATI YA MIPANGO NA FEDHA (BURUDANI, MAAFA NA HUDUMA ZA JAMII)

KAMATI YA UZALISHAJI

KAMATI YA MASOKO NA TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO

WANACHAMA

KATIBU

4.2.2 KAMATI YA MIPANGO NA FEDHA
Kamati ya mipango na fedha itakuwa na wajumbe watatu (3). Mweka hazina atakuwa miongoni mwa hao watu watatu na msimamizi mkuu wa kamati ya mipango na fedha. Wajumbe wawili watatokana na wajumbe sita ambao watachaguliwa na mkutano wa wanakikundi wote. Kamati ya mipango na fedha itakuwa na majukumu yafuatayo:
i. Kuratibu uandaaji wa Mipango, Miradi, na shughuli za Kikundi za
muda mrefu, muda wa kati na mfupi.
ii. Kubuni na kupanga mipango na mikakati ya kutunisha mapato ya kikundi.
iii. Kusimamia kwa karibu zaidi mapato na matumizi yote ya kikundi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa kanuni za usimamizi wa fedha zinafuatwa.
iv. Kusimamia na kuratibu miradi yote ya uzalishaji mali inayomilikiwa na kikundi.
v. Kuratibu mwenendo wa utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu kwa lengo la kuleta ufanisi uliokusudiwa.
vi. Kutoa ushauri kwa vitengo vingine juu ya utekelezaji wa Mipango na shughuli mbalimbali za kikundi.

4.2.3 KAMATI YA UZALISHAJI
Kamati ya Uzalishaji itakuwa na wajumbe watatu (3). Mratibu wa Uzalishaji atakuwa miongoni mwa hao watu watatu na msimamizi mkuu wa kamati ya Uzalishaji. Wajumbe wawili watatokana na wajumbe sita ambao watachaguliwa na mkutano wa wanakikundi wote. Majukumu ya kamati ya uzalishaji ni:
  • Kuhakikisha kuwa program za mafunzo ya mbinu bora za uzalishaji wa mazao zinaanzishwa.
  • Kuhakikisha upatikanaji wa pembejeo kwa wanakikundi ili kuongeza tija katika uzalishaji.
  • Kufuatilia utekelezaji wa maazimio ya wanakikundi juu ya uzalishaji wa mazao.
  • Kuhakikisha kuwa wanakikundi wanafuata mbinu bora za kilimo.

4.2.4 KAMATI YA MASOKO
Kamati ya masoko itakuwa na wajumbe watatu (3). Mratibu wa Masoko atakuwa miongoni mwa hao watu watatu na msimamizi mkuu wa kamati ya Masoko. Wajumbe wawili watatokana na wajumbe sita ambao watachaguliwa na mkutano wa wanakikundi wote. Majukumu ya kamati ya masoko ni:
  • Kuhakikisha kuwa wanakikundi wanakusanya mazao pamoja kwa ajili ya kupata soko la pamoja.
  • Kuhakikisha kuwa mazao yanayokusanywa na wanakikundi kwa ajili ya kuuza yana ubora unaokidhi viwango vya mnunuzi.
  • Kutafuta masoko na kuunganisha wanakikundi na masoko ya bidhaa zinazozalishwa na wanakikundi.
  • Kutafuta taarifa za masoko na kuhakikisha kuwa kikundi kina taarifa za kutosha kuhusu masoko na mahitaji yake.

4.3 UONGOZI WA KIKUNDI
Uongozi wa kikundi utamaanisha ni wale Viongozi waliochaguliwa na wanachama katika Mkutano Mkuu. Hata hivyo kwa upande mwingine itamaanisha pia ni watendaji wa shughuli za kila siku katika kikundi ikihusisha waliochaguliwa na kuajiriwa pale itakapobidi.

4.4 VIONGOZI WA KIKUNDI

Kwa mujibu wa Katiba hii kutakuwa na viongozi wa kuchaguliwa na wanachama kupitia Mkutano wa wanakikundi. Viongozi hao ni pamoja na; Mwenyekiti, Katibu Mtendaji, Mweka Hazina, Mratibu wa Masoko, Mratibu wa Uzalishaji pamoja na Wajumbe wengine sita (6). Wajumbe sita watakaochaguliwa watawajibika katika kamati ndogondogo za kikundi.

4.5 MAJUKUMU YA VIONGOZI WA KIKUNDI
Viongozi wote wa kuchaguliwa na kuteuliwa watakuwa na majukumu ya msingi yafuatayo:-

I. KAZI ZA MWENYEKITI
  • Kusimamia na kuratibu shughuli zote za kikundi.
  • Kuitisha na kuendesha mikutano ya kikundi ikiwa.
  • Kuhakikisha kuwa wanakikundi wote wanashirikishwa katika kufanya maamuzi yanahusu kikundi.
  • Kuhakikisha kuwa katiba ya kikundi inafuatwa.
  • Kuhakikisha kuwa katibu, Mtunza Hazina na wajumbe wengine wanatekeleza wajibu wao ipasavyo.
  • Kuhakikisha kuwa wanakikundi wanalipa michango yao kwa mujibu wa katiba..
  • Kuhakikisha kuwa mipango ya utekelezaji wa shughuli za kikundi inatekelezwa ipasavyo.
  • Kuwakilisha kikundi kwenye mikutano na wadau wengine .

II. KAZI ZA KATIBU MTENDAJI
  • Kuwa mkuu wa timu ya masuala ya kiutawala ya kikundi.
  • Kuweka kumbukumbu za vikao/mikutano yote.
  • Kuweka orodha ya wanachama wote wa Kikundi.
  • Kuitisha mikutano kwa kushauriana na Mwenyekiti kuitisha mikutano.
  • Kuandaa dondoo za mikutano ya kikundi.
  • Kuweka sahihi katika mihutasari iliyoidhinishwa.
  • Kutunza kumbukumbu za vifaa na nyaraka mbalimbali za kikundi.
  • Kuweka sahihi mikataba na malipo yanayohusu kikundi.
  • Kuwa mhimili namba moja (1) wa fedha za kikundi.

III. KAZI ZA MWEKA HAZINA
  • Kuwa mtunza fedha zote za kikundi.
  • Kuandaa na kutoa taarifa za fedha kwa Kamati Tendaji.
  • Kuandaa na kutoa taarifa za fedha kwa Mkutano Mkuu.
  • Kuandaa rasimu ya bajeti ya kila mwaka unaofuata.
  • Kupokea na kujibia hoja za ukaguzi wa mahesabu/taarifa
  • Kutunza kumbukumbu na nyaraka zote muhimu za kifedha.
  • Kudhibiti mali, kusimamia mapato na matumizi ya kikundi.

IV. KAZI ZA MRATIBU WA UZALISHAJI
Kikundi kitakuwa na mratibu wa Uzalishaji ambaye atakuwa na wajibu ufuatao:
  • Kuhakikisha kuwa wanakikundi wanapata mafunzo na stadi zinazohitajika kuzalisha mazao kwa tija.
  • Kupanga na kufuatilia upatikanaji wa pembejeo kwa wanakikundi
  • Kufuatilia upandaji na uvunaji wa mazao kwa wanakikundi .
  • Kusimamia na kufuatilia maamuzi yote yanayofanywa na wanakikundi kuhusu uzalishaji wa mazao.
  • Kufuatilia shughuli zote za pamoja za kikundi zinazohusu uzalishaji wa mazao.
  • Kusimamia upangaji wa malengo ya uzalishaji kwa kikundi na wanakikundi .
  • Kutunza kumbukumbu za uzalishaji mazao kwa kikundi na wanakikundi.

V. KAZI ZA MRATIBU WA MASOKO
  • Kuratibu ukusanyaji wa mazao kwa ajili ya mauzo.
  • Kuhamasisha ukaushaji na uchambuaji wa mazao kwa ajili ya kutimiza mahitaji ya soko.
  • Kuhakikisha kuwa kiasi cha kutosha cha mazao yenye ubora unaotakiwa kinakusanywa.
  • Kutafuta wanunuzi wa mazao na kujadiliana nao juu ya bei, mauzo na mahitaji mengine.
  • Kusimamia mauzo ya mazao na ugawaji wa fedha kwa wanakikundi waliuouza mazao.
  • Kuweka kumbukumbu kuhusu masoko, mauzo, na faida inayotokana na mauzo.

4.6 KIPINDI CHA UONGOZI/VIONGOZI KUWA MADARAKANI.  Uongozi/viongozi wa kikundi cha UMOJA WAKULU WA UKAYAwatakuwa madarakani kwa kipindi cha miaka mitatu (3) mfululizo.
  • Kiongozi yoyote wa kuchaguliwa anaruhusiwa kuwa madarakani kwa vipindi vya awamu tatu (3) kwa nafasi moja na si vinginevyo.

4.7 UKOMO WA UONGOZI / VIONGOZI KUWA MADARAKANI
Kwa mujibu wa Katiba hii, Ukomo wa Uongozi/Kiongozi kuwa madarakani utatokana na kati ya yafuatayo:-
  • Kumalizika kwa kipindi cha uongozi.
  • Kujiuzulu kwa kutoa taarifa ya maandishi ya mwezi mmoja kabla.
  • Kufariki kwa kiongozi/viongozi.
  • Kufukuzwa na/au kuachishwa uongozi.
  • Kutiwa hatiani kwa kosa la jinai na kufungwa jela.
  • Kutokuwa na akili timamu.
  • Kuhama kutoka katika makao makuu ya kikundi kwa kipindi zaidi ya mwaka (1).
  • Kushindwa kutekeleza wajibu na majukumu yake ya kimsingi kama yalivyoainishwa katika Katiba hii.
  • Kutohudhuria vikao vitatu mfulizo vya Kamati za kikundi.

4.8 UCHAGUZI/UTEUZI WA VIONGOZI NA KAMATI

4.8.1 UCHAGUZI /UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI
Viongozi wakuu wa kikundi ambao ni; Mwenyekiti, Katibu Mtendaji, Mweka Hazina, Mratibu wa Uzalishaji, Mratibu wa Masoko pamoja na wajumbe sita watapatikana kwa kuchaguliwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa kikundi. Uchaguzi utafanyika kwenye mkutano wa tatu tangu uongozi uliopo madarakani uchaguliwe isipokuwa kama kutakuwa na sababu za msingi za kufanya uchaguzi.

4.8.2 UCHAGUZI /UTEUZI WA KAMATI MBALIMBALI
Kutakuwa na kamati tendaji, kamati ya mipango na fedha, kamati ya uzalishaji na kamati ya masoko. Wajumbe wa kamati zote za kikundi watachaguliwa kwenye mkutano wa mwaka wa kikundi. Uchaguzi utafanyika kwenye mkutano wa tatu tangu uongozi uliopo madarakani uchaguliwe isipokuwa kama kutakuwa na sababu za msingi za kufanya uchaguzi.
8
4.9 MIKUTANO NA VIKAO VYA KIKUNDI
Kwa mujibu wa Katiba hii, kikundi cha WAKULU WA UKAYA kitakuwa na Mikutano na Vikao vifuatavyo:-

4.9.1 MKUTANO MKUU WA MWAKA
Mkutano huu utakuwa ukifanyika mara moja kila mwaka na kwamba ni sharti ufanyike ndani ya kipindi cha mwezi mmoja tangu kwisha kwa msimu wa mauzo ya mazao. Kila mwaka wa tatu tangu uongozi uliopo madarakani uchaguliwe, Mkutano Mkuu utafanyika sambamba na Uchaguzi wa Viongozi wapya. Wajumbe wa Mkutano Mkuu watakuwa ni viongozi na wanachama wote wa kikundi, Mkutano Mkuu wa mwaka pamoja na masuala mengine, utakuwa na kazi na/au majukumu ya msingi yafuatayo:-
i. Kusoma, kupokea, kujadili na kupitisha taarifa za utekelezaji mipango
ya maendeleo ya kikundi
ii. Kusoma, kupokea, kujadili na kupitisha taarifa za utekelezaji na mapato na matumizi ya fedha za kikundi.
iii. Kusoma, kupokea, kujadili na kupitisha Mpango wa Mapato na Matumizi ya kikundi kwa mwaka unaofuata.
iv. Kujadili na kutathmini ushiriki wa wanakikundi kwenye utekelezaji wa mipango na makubaliano ya kikundi.
v. Kutafakari, kujadili na kufanya mapitio (marekebisho) ya Katiba ya kikundi pale itakapobidi.
vi. Pamoja na majukumu mengine yanayotekelezwa sambamba na Mkutano Mkuu wa kawaida wa kila mwaka, Mkutano Mkuu wa mwaka wa tatu wa muhula wa uongozi utapaswa kuchagua na kuthibitisha viongozi pamoja na kusoma, kupokea, kujadili na kupitisha taarifa ya utekelezaji na fedha kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi.
vii. Kutoa maamuzi ya kuchukuliwa kwa hatua za kinidhamu kwa viongozi na wanakikundi waliokiuka maadili ya kikundi kwa mujibu wa Katiba hii.

4.9.2 MKUTANO MKUU MAALUMU / DHARULA
Mikutano yote maalumu au dharula itafanyika kutokana na sababu maalumu au dharula ambayo imejitokeza na kwamba wajumbe wa Mikutano hiyo watakuwa ni viongozi na wanakikundi wote.

4.9.3 MKUTANO WA ROBO MWAKA
Mkutano wa robo mwaka utafanyika mara moja kila baada ya miezi mitatu (3) au robo mwaka. Wajumbe wa mkutano wa robo mwaka watakuwa ni viongozi na wanachama wote kikundi. Mkutano wa robo mwaka utapokea taarifa za fedha na utekelezaji, kuzijadili, kuzithibitisha na kufanya tathmini juu ya mwenedo wa kikundi. Mkutano wa robo mwaka utakuwa na majukumu yafuatavo:-
  • Kusoma, kupokea, kujadili na kuthibitisha taarifa za utekelezaji na fedha za kila baada ya miezi mitatu (robo mwaka)
  • Kupokea, kuijadili na kuipitisha mipango ya maendeleo ya kikundi.
  • Kupokea, kujadili na kupitisha/kutopitisha maombi ya wanachama wapya.
  • Kupokea na kuufanyia kazi ushauri wa kitaalamu/kiufundi unaotolewa na wataalamu wa kiufundi.
  • Kufanya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa kawaida muda unapokaribia wa kufanyika na Mkutano Mkuu maalumu/dharula unapohitajika.
  • Kutathmini mwenendo wa utendaji wa viongozi pamoja na wanakikundi kwa uwazi, ukweli na haki.
  • Kuandaa na kuwasilisha mapendekezo ya maboresho/marekebisho ya Katiba kwenye Mkutano Mkuu wa kawaida.

4.9.4 VIKAO VYA KAMATI
Vikao vya Kamati zote vitafanyika mara moja kila mwezi na kwamba vikao vitakuwa vikifanya mapitio ya mara kwa mara kuhusu utekelezaji wa Mipango na Shughuli za kikundi. Majukumu ya kamati yatakuwa ni kama yalivyoainishwa kwenye kipengele 4.2 hapo juu.

4.10 TAARIFA ZA MIKUTANO NA VIKAO
  • Mikutano yote ni sharti itolewe taarifa ya kufanyika si pungufu ya siku kumi na nne (14) kabla ya kufanyika na agenda zilizopendekezwa ni sharti zibainishwe na mlango utakuwa wazi kwa siku saba (7) zaidi ili wenye agenda nyingine tofauti na zilizopendekezwa waweze kuziwasilisha kwa Katibu Mtendaji kwa uchambuzi na mapitio kabla ya kuingizwa kwenye ajenda za mikutano/vikao.
  • Vikao vya Kamati zote vinaweza kuitishwa kufanyika kulingana na mahitaji pasipo kigezo cha kutoa taarifa rasmi katika kipindi fulani.
  • Mihtasari yote ya vikao na/au mikutano itaandaliwa na kusomwa kwenye mkutano au kikao kinachofuata.

4.11 IDADI YA WAJUMBE WANAOHALALISHA MKUTANO / KIKAO
Kikao au Mkutano wowote utaweza kufanyika pale utakapokuwa na idadi ya wajumbe waliotarajiwa kuhudhuria kufikia nusu (1/2) na kuendelea.

4.12 TARATIBU ZA UPIGAJI KURA KATIKA CHAGUZI
i. Katika uchaguzi wowote utakaofanyika ni sharti kuwa, kura zote zitapigwa kwa siri.
ii. Kila mjumbe atakuwa na haki ya kupiga kura moja kwa mgombea mmoja.
iii. Endapo itatokea kura kulingana mara mbili mfululizo, basi Mwenyekiti ana haki ya kutumia kura ya turufu ili mshindi aweze kupatikana.
iv. Ili mgombea yoyote ikiwa pamoja na nafasi ya Mwenyekiti aweze kuchaguliwa na kutangazwa mshindi basi ni sharti apate kura zaidi ya wagombea wengine wote.

10.SEHEMU YA TANO

MASUALA YA KIFEDHA KATIKA KIKUNDI

5.1 VYANZO VYA MAPATO YA KIKUNDI
Kwa mujibu wa Katiba hii vyanzo vya mapato ya kikundi ni kama ifuatavyo:-
i. Viingilio vya uanachama.
ii. Ada ya kila mwaka ya uanachama.
iii. Ruzuku mbalimbali.
iv. Miradi ya Uzalishaji mali.
v. Michango ya hiari toka kwa wanachana na wadau wengine.
vi. Misaada kutoka nje ya kikundi.
viii. Mikopo kutoka taasisi za kifedha.
Michango yo yote itapokelewa na kukatiwa stakabadhi ili kuthibitisha na kukiri kupokea mchango/michango hiyo.

5.2 KIINGILIO, ADA NA MICHANGO MBALIMBALI
Kutakuwa na Kiingilio cha Uanachama, Ada ya uanachama ya mwaka pamoja na michango mbalimbali ambayo wanachama watakuwa wakihitajika kutoa baada ya kukubalika kupitia vikao halali vya kikundi. Viwango vya michango hiyo vitakuwa kama ifuatavyo:-
i. Kiingilio cha Uanachama
Kiwango cha Kiingilio cha uanachama kwa mtu anayehitaji kujiunga na kikundi binafsi kitakuwa ni Shilingi Elfu Thelathini za Kitanzania (TSZ. 30,000/=)
ii. Ada ya Uanachama ya Mwezi
Kiwango cha ada ya mwezi kwa mwanachama kitakuwa ni shilingi elfu kumi za kitanzania (TSZ. 10,000/=) tu.
ii. Michango ya Hiari
Kutakuwa na michango ya hiari ambayo mtu hatolazimishwa bali anaweza kujitolea mali au fedha kwa mapenzi yake mwenyewe na kwa lengo la kukijenga na kukiendeleza kikundi.

11 SEHEMU YA SITA


USIMAMIZI WA MALI NA RASLIMALI

6.1 USIMAMIZI WA VIFAA
Mali na raslimali zote za kikundi zitasimamiwa kwa kuhakikisha yanafanyika yafuatayo:-
i. Mali na raslimali zote zitaorodheshwa katika Regista maalum.
ii. Mali zote na raslimali zitawekwa alama/namba ya utambulisho.

6.2 USIMAMIZI WA FEDHA
  • Kutakuwa na Akaunti za Akiba na Hundi katika Benki.
  • Akaunti za kikundi zitafunguliwa katika Benki kati ya CRDB ua Benki zilizopo karibu na makao makuu ya kikundi.
  • Watia sahihi (Bank Signatories) katika akaunti zote watathibitishwa na wanakikundi. Kutakuwa na makundi mawili ya watia sahihi:-
Kundi A.
Katibu Mtendaji
Mwenyekiti.
Kundi B
Mweka Hazina
Mjumbe mmoja wa kamati ambayo siyo ya fedha (KE)
  • Wawili kati yao wataruhusiwa kuchukua fedha kutoka akaunti yoyote iliyopo katika Benki yoyote (mmoja kutoka kila kundi la A na B). Endapo dharula itajitokeza watia sahihi wote wawili wa kundi B hawapo, basi watia sahihi wawili wa kundi A wanaweza kuchukua fedha na si kinyume chake
  • Matumizi yoyote ya kikundi ni lazima yapitishwe na kikundi. Fedha hazitachukuliwa benki bila kuidhinishwa kwenye kikao cha wanakikundi au kamati tendaji.
  • Mwaka wa fedha wa kikundi utaanzia kila mwezi Julai na kuishia Juni ya mwaka unaofuata.

12.SEHEMU YA SABA

MASUALA MENGINEYO

7.1. MASUALA MUHIMU YA KISHERIA
Masuala mengine ya kisheria na kanuni katika kikundi ni pamoja na:-
  • Kikundi kitaenendesha shughuli zake kwa lugha za Kiswahili.
  • Kamati tendaji ina haki ya kutoa mapendekezo ya kubadilisha viwango vya kiingilio na ada pamoja na vipengele vya Katiba na kuwasilisha kwenye Mkutano Mkuu kwa mjadala na maamuzi ya mwisho.
  • Kikundi kitakuwa tayari kupokea misaada, ruzuku na mikopo toka kwa wafadhili na/au wahisani ikiwa tu misaada, ruzuku na mikopo hiyo inaendana na malengo na masharti ya kikundi kwa mujibu wa Katiba hii.
  • Jambo lolote ambalo litaleta utata wa kitafsiri ndani na nje ya Katiba hii, basi tafsiri sahihi itatolewa au kuamuliwa na wanakikundi wenyewe.
  • Kikundi kina haki ya kushitaki au kushitakiwa kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

7.2 MWAKA WA KIKUNDI
Mwaka wa kikundi utakuwa kuanzia 01/01 hadi 31/12/

7.3 KUFA / KUSAMBARATIKA KWA KIKUNDI
Kikundi cha UMOJA WA WAKULU WA UKAYA kipo kwa ajili ya kuwasaidia na kuwawezesha wanakikundi kujiendeleza kiuchumi. Kutokana na malengo yake inategemewa kuonekana kuwa kikundi ni endelevu. Hata hivyo endapo kikundi kitasambaratika mali ya kikundi itawekwa chini ya uangalizi wa serikali ya wilaya ambacho kikundi kipo. Serikali ngazi ya wilaya itasimamia ugawanyaji wa mali kwa wanakikundi pale itakapobidi na kama kuna rasilimali zilizotokana na wafadhili rasilimali hizo zitapewa taasisi nyingine inayofanya kazi za maendeleo zinazofanana na kikundi hiki. Hata hivyo Serikali haitakuwa na mamlaka ya kuingilia shughuli za kiutendaji za kikundi wakati wote wa uhai wake isipokuwa itakapohitajiwa msaada wa kufanya hivyo.
7.3 UTATUZI WA MIGOGORO Kikundi cha UMOJA WA WAKULU WA UKAYA kitatua migogoro kwa kufuata sheria zake za ndani na taratibu zilizowekwa.Hata hivyo umoja utafuata shriea z anchi pale inapobidi.

7.4 MABADILIKO YA KATOBA 7.4.1 Mabadiliko yoyote ya Katiba ya UMOJA WA WAKULU WA UKAYA lazima yaanie kwa wanachama wa UMOJA HUU na yawe kwa manufaa ya umoja na jamii kwa ujumla.

7.4.2 Waraka wa mapendekezo ya kubadili katiba yanatakiwa kuwasilishwa kwa meneykiti kwa maandishi miezi miwili kabla ya mkutano mkuu wa UMOJA na kupitishwa na utawala.Katibu wa bodi amabaye ni mwenyekiti wa UMOJA tawajulisha wanachama mapendekezo ya marekebishon yaliyowasilishwa mwezi mmoja kabla ya mkutano mkuu. 7.4.3 Bodi itakuwa ndio mamalaka ya kutasfsir katiba au sheria za Umoja.Na kwa Msingi huuo maamuzi ya Bodi yatakuwa ndio maamuiz ya mwisho.
13
KATIBA HII IMEKUBALIWA NA KUPITISHWA RASMI NA
WANACHAMA WAANZILISHI LEO TAREHE ……………………………….
……………………………..… ………………………………
SAHIHI YA MWENYEKITI SAHIHI YA KATIBU MTENDAJI

No comments:

Post a Comment