KATIBA YA
KIKUNDI
WAKULU WA
UKAYA
(WAWAU)
TOLEO LA KWANZA
S.L.P 92
IMEANDALIWA
Mahali - Gairo
AGOSTI,
2014.
KATIBA YA KIKUNDI CHA WAKULU WA UKAYA
SEHEMU YA
KWANZA
TAARIFA ZA KIKUNDI
1.1.
JINA LA KIKUNDI.
WAKULU WA
UKAYA
1.2.
MAKAO MAKUU YA KIKUNDI
Makao makuu ya kikundi yatakuwa Gairo ila yanaweza kubadilika pale
inapobidi
1.3.
ANUANI ZA ASASI
Kwa sasa anuani ya kikundi itakuwa ni:-
Jina la Kikundi WAKULU WA UKAYA
S.L.P- 92
Mahali - Gairo
1.4.
ENEO LA SHUGHULI ZA KIKUNDI
Kikundi hiki kitaendesha shughuli zake kwenye wilaya ya Gairo, na pale
inapobidi kikundi kinaweza kupanua shughuli zake na kuifikia wilaya zingine.
1.5.
WALENGWA NA WANUFAIKA WA KIKUNDI
Walengwa
wa kikundi au umoja huu ni watu wote wenye asili/wazawa wa ukanda wa ukagulu
ambao watakuwa tayari kujiunga na kikundi kwa kukubaliana na masharti na kanuni
za kikundi hiki pamoja na katiba yake.Pamoja
na kuwa tayari kujishughulisha na maendeleo ya Gairo katika nyanja za
afya,elimu,utamaduni na uchumi.
1.6.
NEMBO NA MUHURI WA KIKUNDI
Kikundi kitakuwa na nembo
ambayo ni mduara wenye mlima, moto na watu ndani yake ambao wanalima kwa pamoja.
SEHEMU YA PILI
MALENGO YA KIKUNDI
2.1 DIRA NA DHAMIRA KUU
DIRA
Kuwa
na umoja thabiti na imara wa wakazi wote Gairo wa ndani na nje ya nchi
wanaopendana, shirikiana na kushiriki kikamilifu kuinua ukagulu kujiletea
maendeleo katika nyanja zote za maendeleo endelevu ya Kiuchumi, Kielimu, Kiafya na Kiutamaduni.
DHAMIRA KUU
Kuhakikisha kuwa umoja thabiti na imara ili kujenga jamii ya wakagulu
wanaopendana, shirikiana na kushiriki katika nyanja zote za maendeleo endelevu ya
Kiuchumi, Kielimu, Kiafya na Kiutamaduni.
2.2 MADHUMUNI YA KIKUNDI
Kikundi cha WAKULU WA UKAYA kitakuwa na madhumuni ya msingi yafuatayo:-
- Kuongeza
ari na hamasa ya wanakikundi na jamii kupiga vita umaskini wa kipato na ukosefu
wa chakula.
- Kusaidiana
wakati wa sherehe,majanga na vifo.
- Kusaidia
na kuwezesha wanakikundi na jamii katika kuzitambua na kuzitumia kikamilifu fursa za kujiendeleza
kupitia kilimo cha mahindi, maharage, viazi na mazao mengineyo.
- Kusaidia
jamii kupata stadi na mbinu bora za kilimo, usindikaji kuongeza ubora wa
mazao, na upatikanaji wa pembejeo ili kuinua uzalishaji wa mazao.
- Kuwezesha
wanakikundi na jamii kiujumla kupata stadi na mbinu za kuwa wenyeji/wazawa
mahiri.
- Kusaidia
wanakikundi na jamii kwa ujumla katika kutafuta na kujiunga na masoko ya
kuaminika ya bidhaa zinazozalishwa katika kilimo.
- Kuchochea
michezo kama njia ya kujenga umoja na mshikamano.
SEHEMU YA TATU
UANACHAMA KATIKA KIKUNDI
3.1
SIFA ZA WANACHAMA WA KIKUNDI
Uanachama katika kikundi
cha WAKULU WA UKAYA ni kwa kila mtu ambaye ni raia wa Tanzania, mwenye akili
timamu, mwenye utayari na aliye na
mtazamo wa kujisaidia na kujiwezesha pamoja na kuwawezesha wengine kujiletea
maendeleo endelevu katika nyanja za Kilimo, Kibiashara na Kiuchumi kwa ujumla.
Kila mwanachama ni sharti awe amesoma Katiba hii na kuielewa vyema na
kukubaliana na masharti, taratibu, kanuni na maelekezo yaliyomo katika katiba
hii na kuilinda bila haya.
3.2
AINA ZA WANACHAMA WA KIKUNDI
Kikundi cha WAKULU WA UKAYA kitakuwa na wanachama wa aina moja tu ambao
ni:-
i.
Uanachama wa mtu mmoja
mmoja mwenye ari ya kujituma na kujitolea na hamasa ya kujiwezesha pamoja na
kuwawezesha wengine kupata maendeleo.
3.3
NAMNA YA KUJIUNGA UANACHAMA WA KIKUNDI
Mtu anayehitaji kujiunga na unachama katika kikundi cha WAKULU WA UKAYA atapaswa
kuandika barua kwa Kamati ya Utendaji kuomba kujiunga au kujaza fomu ya
kukubali kujiunga na kikundi. Kikundi kitajadili na kumjulisha muombaji kuhusu
maamuzi yaliyofikiwa.
3.4
HAKI ZA MWANAKIKUNDI
Kwa mujibu wa Katiba hii
kila mwanakikundi atakuwa na haki za msingi kama zifuatavyo:-
- Kuwasiliana
na uongozi/viongozi na kupokea taarifa za kikundi.
- Kuhudhuria
na kuwakilishwa katika mikutano/vikao tofauti.
- Kuchagua
na/au kuchaguliwa kuwa kiongozi wa kikundi. Mwombaji yeyote wa uongozi
atapaswa kujaza fomu ya kuomba nafasi ya uongozi.
- Kupiga
kura moja katika kila uchaguzi.
- Kujieleza
na kujitetea katika kikundi.
- Kujengewa
uwezo na kikundi kutokana na shughuli mbalimbali kama vile mafunzo na
huduma nyinginezo zinazotolewa na kikundi kwa ajili ya maendeleo ya
wanakikundi.
- Kutumia
mali za kikundi kwa kufuata utaratibu uliopo.
3.5
WAJIBU WA MWANAKIKUNDI
Kila mwanakikundi atakuwa
na wajibu wa msingi katika kikundi cha Wakulu wa Ukaya ni kama ifuatavyo:-
- Kuhudhuria
vikao na mikutano mbalimbali ya kikundi.
- Kulipa
ada na michango mbalimbali ya kikundi.
- Kushiriki
katika utekelezaji shughuli na mipango ya kuimarisha na kuendeleza
kikundi.
- Kujitoa
na kujitolea kwa ajili ya ufanisi na maendeleo ya kikundi.
- Kuheshimu
na kutoa ushirikiano unaohitajika kwa uongozi/viongozi waliopo madarakani
kwa manufaa ya kikundi.
- Kutafuta
habari na taarifa muhimu zitakazosaidia kuimarisha na kuendeleza kikundi.
3.6
KUKOMA UANACHAMA KATIKA KIKUNDI
Uanachama wa kikundi
unaweza kukoma kwa msukumo wa kikundi au mwanakikundi mwenyewe. Mwanakikundi
anapoamua kukomesha uanachama wake atawajibika kulipa madeni yake kwa kikundi
kabla ya kukubaliwa kujitoa kwenye kikundi. Mwanakikundi anaweza kukoma
uanachama ikiwa yatatokea miongoni mwa mambo yafuatayo:-
- Mwanakikundi
kuacha kwa hiyari yake mwenyewe Mwanakikundi atapaswa kutoa taarifa ya
maandishi ya mwezi mmoja na kurudisha mali zote za kikundi.
- Mwanakikundi
kushindwa kulipa ada ya mwaka kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo.
- Mwanakikundi
kwenda kinyume na maadili ya kikatiba ya kikundi, kikundi kitamwondoa kwa
maamuzi ya uongozi wa juu.
- Mtu
akifariki au kikundi kikisambaratika
- Mwanakikundi
itakapobainika na kuthibitika ametumia jina la kikundi/mali za kikundi
kisiasa au kwa namna yoyote kukihusisha kikundi katika siasa au mambo yake
binafsi yasio na maslahi na mlengo wa kikundi.
- Ikitokea mwanakikundi
yeyote atafariki basi watarudishiwa ada na hisa zake kwa wategemezi.
- Mwanakikundi
kutohudhuria mikutano mikuu ya kikundi kwa mara tatu mfululizo bila
taarifa.
Endapo mwanakikundi atakoma
uanachama kwa sababu zilizoorodheshwa hapo juu, hatarudishiwa kiingilio, ada na
hakuna haki ya kudai au kupewa mali yoyote, isipokuwa tu mwanachama amefariki
na hakuwa nadeni kwenye kikundi.
SEHEMU YA
NNE
UONGOZI, UENDESHAJI NA USIMAMIZI WA KIKUNDI
4.1
MUUNDO WA KIKUNDI
|
Muundo wa kikundi cha WAKULU WA UKAYAutakuwa ni kama ifuatavyo:-
4.2
KAMATI ZA KIKUNDI
Kikundi kitakuwa na kamati
nne muhimu ambazo zitasaidia uendeshaji
na usimamizi wa shughuli za kikundi. Kamati hizo ni:
·
Kamati tendaji.
·
Kamati ya Mipango na fedha.
·
Kamati ya Uzalishaji na
·
Kamati ya Masoko.
4.2.1
KAMATI TENDAJI YA KIKUNDI
Kamati tendaji ya kikundi
ndiyo msimamizi mkuu wa kila siku wa masuala yote ya kikundi. Kamati tendaji
itaundwa na watu saba ambao ni mwenyekiti, katibu, mweka hazina, mratibu wa
uzalishaji na mratibu wa masoko na wanachama wawili watakaowakilisha wanachama
wengine.Majukumu ya kamati tendaji yatakuwa ni:
i. Kuandaa Kanuni, Sheria
na Taratibu mbalimbali vitakavyotumika kuendesha kikundi na kuwasilisha kwa
wanakikundi kwa majadiliano na makubaliano. Kanuni yoyote haitakubalika na
kikundi isipouwa pale tu itakapopitishwa na wanachama kwenye mkutano mkuu.
ii.
Kusimamia shughuli za
kila siku za kikundi.
iii.
Kuandaa, Kuratibu,
kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Mipango,
Programu na/au Shughuli zinazofanywa na kikundi.
iv.
Kufanya tathmini ya kiuwezo
kwa kamati za Uzalishaji, masoko
pamoja na Mipango na fedha na kupima uendeshaji na maendeleo ya kikundi
kila baada ya miezi mitatu (3).
v.
Kutoa taarifa za tathmini
za kiuwezo wa kikundi na kutoa ushauri na
mapendekezo kwa Kamati husika na wanakikundi juu ya mwenendo wa kikundi
kiujumla.
vi.
Kuandaa taarifa za
utendaji, utekelezaji na maendeleo ya kikundi na
kuwasilisha kwa
wanakikundi kwenye mkutano mkuu wa kikundi.
4.2.2
KAMATI YA MIPANGO NA FEDHA
Kamati ya mipango na fedha itakuwa na wajumbe watatu (3). Mweka hazina
atakuwa miongoni mwa hao watu watatu na msimamizi mkuu wa kamati ya mipango na
fedha. Wajumbe wawili watatokana na wajumbe sita ambao watachaguliwa na mkutano
wa wanakikundi wote. Kamati ya mipango na fedha
itakuwa na majukumu yafuatayo:
i.
Kuratibu uandaaji wa
Mipango, Miradi, na shughuli za Kikundi za
muda mrefu, muda wa kati na mfupi.
ii.
Kubuni na kupanga mipango
na mikakati ya kutunisha mapato ya kikundi.
iii.
Kusimamia kwa karibu
zaidi mapato na matumizi yote ya kikundi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa
kanuni za usimamizi wa fedha zinafuatwa.
iv.
Kusimamia na kuratibu
miradi yote ya uzalishaji mali inayomilikiwa na kikundi.
v.
Kuratibu mwenendo wa utekelezaji
wa Sheria, Kanuni na Taratibu kwa lengo la kuleta ufanisi uliokusudiwa.
vi.
Kutoa ushauri kwa vitengo
vingine juu ya utekelezaji wa Mipango na shughuli mbalimbali za kikundi.
4.2.3
KAMATI YA UZALISHAJI
Kamati ya Uzalishaji
itakuwa na wajumbe watatu (3). Mratibu wa Uzalishaji atakuwa miongoni mwa hao
watu watatu na msimamizi mkuu wa kamati ya Uzalishaji. Wajumbe wawili
watatokana na wajumbe sita ambao watachaguliwa na mkutano wa wanakikundi wote.
Majukumu ya kamati ya uzalishaji ni:
·
Kuhakikisha kuwa program za
mafunzo ya mbinu bora za uzalishaji wa mazao zinaanzishwa.
·
Kuhakikisha upatikanaji wa
pembejeo kwa wanakikundi ili kuongeza tija katika uzalishaji.
·
Kufuatilia utekelezaji wa
maazimio ya wanakikundi juu ya uzalishaji wa mazao.
·
Kuhakikisha kuwa wanakikundi
wanafuata mbinu bora za kilimo.
4.2.4
KAMATI YA MASOKO
Kamati ya masoko itakuwa na
wajumbe watatu (3). Mratibu wa Masoko atakuwa miongoni mwa hao watu watatu na
msimamizi mkuu wa kamati ya Masoko. Wajumbe wawili watatokana na wajumbe sita
ambao watachaguliwa na mkutano wa wanakikundi wote. Majukumu ya kamati ya masoko ni:
·
Kuhakikisha kuwa
wanakikundi wanakusanya mazao pamoja kwa ajili ya kupata soko la pamoja.
·
Kuhakikisha kuwa mazao
yanayokusanywa na wanakikundi kwa ajili ya kuuza yana ubora unaokidhi viwango
vya mnunuzi.
·
Kutafuta masoko na
kuunganisha wanakikundi na masoko ya bidhaa zinazozalishwa na wanakikundi.
·
Kutafuta taarifa za masoko
na kuhakikisha kuwa kikundi kina taarifa za kutosha kuhusu masoko na mahitaji
yake.
4.3
UONGOZI WA KIKUNDI
Uongozi wa kikundi
utamaanisha ni wale Viongozi waliochaguliwa na wanachama katika Mkutano Mkuu.
Hata hivyo kwa upande mwingine itamaanisha pia ni watendaji wa shughuli za kila
siku katika kikundi ikihusisha waliochaguliwa na kuajiriwa pale itakapobidi.
4.4
VIONGOZI WA KIKUNDI
Kwa mujibu wa Katiba hii
kutakuwa na viongozi wa kuchaguliwa na wanachama kupitia Mkutano wa
wanakikundi. Viongozi hao ni pamoja na; Mwenyekiti, Katibu Mtendaji, Mweka
Hazina, Mratibu wa Masoko, Mratibu wa Uzalishaji pamoja na Wajumbe wengine sita
(6). Wajumbe sita watakaochaguliwa watawajibika katika kamati ndogondogo za
kikundi.
4.5
MAJUKUMU YA VIONGOZI WA KIKUNDI
Viongozi wote wa kuchaguliwa na kuteuliwa watakuwa na majukumu ya
msingi yafuatayo:-
I.
KAZI ZA MWENYEKITI
- Kusimamia
na kuratibu shughuli zote za kikundi.
- Kuitisha
na kuendesha mikutano ya kikundi ikiwa.
- Kuhakikisha
kuwa wanakikundi wote wanashirikishwa katika kufanya maamuzi yanahusu
kikundi.
- Kuhakikisha
kuwa katiba ya kikundi inafuatwa.
- Kuhakikisha
kuwa katibu, Mtunza Hazina na wajumbe wengine wanatekeleza wajibu wao
ipasavyo.
- Kuhakikisha
kuwa wanakikundi wanalipa michango yao kwa mujibu wa katiba..
- Kuhakikisha
kuwa mipango ya utekelezaji wa shughuli za kikundi inatekelezwa ipasavyo.
- Kuwakilisha
kikundi kwenye mikutano na wadau wengine .
II.
KAZI ZA KATIBU MTENDAJI
- Kuwa
mkuu wa timu ya masuala ya kiutawala ya kikundi.
- Kuweka
kumbukumbu za vikao/mikutano yote.
- Kuweka
orodha ya wanachama wote wa Kikundi.
- Kuitisha
mikutano kwa kushauriana na Mwenyekiti kuitisha mikutano.
- Kuandaa
dondoo za mikutano ya kikundi.
- Kuweka
sahihi katika mihutasari iliyoidhinishwa.
- Kutunza
kumbukumbu za vifaa na nyaraka mbalimbali za kikundi.
- Kuweka
sahihi mikataba na malipo yanayohusu kikundi.
- Kuwa
mhimili namba moja (1) wa fedha za kikundi.
III.
KAZI ZA MWEKA HAZINA
- Kuwa
mtunza fedha zote za kikundi.
- Kuandaa
na kutoa taarifa za fedha kwa Kamati Tendaji.
- Kuandaa na kutoa taarifa za fedha kwa
Mkutano Mkuu.
- Kuandaa
rasimu ya bajeti ya kila mwaka unaofuata.
- Kupokea
na kujibia hoja za ukaguzi wa mahesabu/taarifa
- Kutunza
kumbukumbu na nyaraka zote muhimu za kifedha.
- Kudhibiti
mali, kusimamia mapato na matumizi ya kikundi.
IV.
KAZI ZA MRATIBU WA UZALISHAJI
Kikundi kitakuwa na mratibu
wa Uzalishaji ambaye atakuwa na wajibu ufuatao:
- Kuhakikisha
kuwa wanakikundi wanapata mafunzo na stadi zinazohitajika kuzalisha mazao
kwa tija.
- Kupanga
na kufuatilia upatikanaji wa pembejeo kwa wanakikundi
- Kufuatilia
upandaji na uvunaji wa mazao kwa wanakikundi .
- Kusimamia
na kufuatilia maamuzi yote yanayofanywa na wanakikundi kuhusu uzalishaji
wa mazao.
- Kufuatilia
shughuli zote za pamoja za kikundi zinazohusu uzalishaji wa mazao.
- Kusimamia
upangaji wa malengo ya uzalishaji kwa kikundi na wanakikundi .
- Kutunza
kumbukumbu za uzalishaji mazao kwa kikundi na wanakikundi.
V.
KAZI ZA MRATIBU WA MASOKO
·
Kuratibu ukusanyaji wa
mazao kwa ajili ya mauzo.
·
Kuhamasisha ukaushaji na
uchambuaji wa mazao kwa ajili ya kutimiza mahitaji ya soko.
·
Kuhakikisha kuwa kiasi cha
kutosha cha mazao yenye ubora unaotakiwa kinakusanywa.
·
Kutafuta wanunuzi wa mazao
na kujadiliana nao juu ya bei, mauzo na mahitaji mengine.
·
Kusimamia mauzo ya mazao na
ugawaji wa fedha kwa wanakikundi waliuouza mazao.
·
Kuweka kumbukumbu kuhusu
masoko, mauzo, na faida inayotokana na mauzo.
4.6
KIPINDI CHA UONGOZI/VIONGOZI KUWA MADARAKANI.
- Uongozi/viongozi
wa kikundi cha WAKULU WA UKAYAwatakuwa madarakani kwa kipindi cha miaka
mitatu (3) mfululizo.
- Kiongozi
yoyote wa kuchaguliwa anaruhusiwa kuwa madarakani kwa vipindi vya awamu
tatu (3) kwa nafasi moja na si vinginevyo.
4.7
UKOMO WA UONGOZI / VIONGOZI KUWA MADARAKANI
Kwa mujibu wa Katiba hii,
Ukomo wa Uongozi/Kiongozi kuwa madarakani utatokana na kati ya yafuatayo:-
- Kumalizika
kwa kipindi cha uongozi.
- Kujiuzulu
kwa kutoa taarifa ya maandishi ya mwezi mmoja kabla.
- Kufariki
kwa kiongozi/viongozi.
- Kufukuzwa
na/au kuachishwa uongozi.
- Kutiwa
hatiani kwa kosa la jinai na kufungwa jela.
- Kutokuwa
na akili timamu.
- Kuhama
kutoka katika makao makuu ya kikundi kwa kipindi zaidi ya mwaka (1).
- Kushindwa
kutekeleza wajibu na majukumu yake ya kimsingi kama yalivyoainishwa katika
Katiba hii.
- Kutohudhuria
vikao vitatu mfulizo vya Kamati za kikundi.
4.8
UCHAGUZI/UTEUZI WA VIONGOZI NA KAMATI
4.8.1 UCHAGUZI /UTEUZI WA
VIONGOZI MBALIMBALI
Viongozi wakuu wa kikundi
ambao ni; Mwenyekiti, Katibu Mtendaji, Mweka Hazina, Mratibu wa Uzalishaji,
Mratibu wa Masoko pamoja na wajumbe sita watapatikana kwa kuchaguliwa na
wajumbe wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa kikundi. Uchaguzi utafanyika kwenye mkutano
wa tatu tangu uongozi uliopo madarakani uchaguliwe isipokuwa kama kutakuwa na
sababu za msingi za kufanya uchaguzi.
4.8.2 UCHAGUZI /UTEUZI WA KAMATI
MBALIMBALI
Kutakuwa na kamati tendaji,
kamati ya mipango na fedha, kamati ya uzalishaji na kamati ya masoko. Wajumbe
wa kamati zote za kikundi watachaguliwa kwenye mkutano wa mwaka wa kikundi.
Uchaguzi utafanyika kwenye mkutano wa tatu tangu uongozi uliopo madarakani
uchaguliwe isipokuwa kama kutakuwa na sababu za msingi za kufanya uchaguzi.
4.9
MIKUTANO NA VIKAO VYA KIKUNDI
Kwa mujibu wa Katiba hii,
kikundi cha WAKULU WA UKAYA kitakuwa na Mikutano na Vikao vifuatavyo:-
4.9.1 MKUTANO MKUU WA MWAKA
Mkutano huu utakuwa
ukifanyika mara moja kila mwaka na kwamba ni sharti ufanyike ndani ya kipindi
cha mwezi mmoja tangu kwisha kwa msimu wa mauzo ya mazao. Kila mwaka wa tatu
tangu uongozi uliopo madarakani uchaguliwe, Mkutano Mkuu utafanyika sambamba na
Uchaguzi wa Viongozi wapya. Wajumbe wa Mkutano Mkuu watakuwa ni viongozi na
wanachama wote wa kikundi, Mkutano Mkuu wa mwaka pamoja na masuala mengine,
utakuwa na kazi na/au majukumu ya msingi yafuatayo:-
i. Kusoma, kupokea,
kujadili na kupitisha taarifa za utekelezaji mipango
ya maendeleo ya kikundi
ii.
Kusoma, kupokea, kujadili
na kupitisha taarifa za utekelezaji na mapato na matumizi ya fedha za kikundi.
iii.
Kusoma, kupokea, kujadili
na kupitisha Mpango wa Mapato na Matumizi ya kikundi kwa mwaka unaofuata.
iv.
Kujadili na kutathmini
ushiriki wa wanakikundi kwenye utekelezaji wa mipango na makubaliano ya
kikundi.
v.
Kutafakari, kujadili na
kufanya mapitio (marekebisho) ya Katiba ya kikundi pale itakapobidi.
vi.
Pamoja na majukumu mengine
yanayotekelezwa sambamba na Mkutano Mkuu wa kawaida wa kila mwaka, Mkutano Mkuu
wa mwaka wa tatu wa muhula wa uongozi utapaswa kuchagua na kuthibitisha viongozi pamoja na kusoma,
kupokea, kujadili na kupitisha taarifa ya utekelezaji na fedha kwa kipindi cha
miaka mitatu ya uongozi.
vii.
Kutoa maamuzi ya
kuchukuliwa kwa hatua za kinidhamu kwa viongozi na wanakikundi waliokiuka
maadili ya kikundi kwa mujibu wa Katiba hii.
4.9.2 MKUTANO MKUU MAALUMU /
DHARULA
Mikutano yote maalumu au
dharula itafanyika kutokana na sababu maalumu au dharula ambayo imejitokeza na
kwamba wajumbe wa Mikutano hiyo watakuwa ni viongozi na wanakikundi wote.
4.9.3 MKUTANO WA ROBO MWAKA
Mkutano wa robo mwaka
utafanyika mara moja kila baada ya miezi mitatu (3) au robo mwaka. Wajumbe wa
mkutano wa robo mwaka watakuwa ni viongozi na wanachama wote kikundi. Mkutano
wa robo mwaka utapokea taarifa za fedha na utekelezaji, kuzijadili,
kuzithibitisha na kufanya tathmini juu ya mwenedo wa kikundi. Mkutano wa robo mwaka utakuwa na majukumu yafuatavo:-
- Kusoma,
kupokea, kujadili na kuthibitisha taarifa za utekelezaji na fedha za kila
baada ya miezi mitatu (robo mwaka)
- Kupokea,
kuijadili na kuipitisha mipango ya maendeleo ya kikundi.
- Kupokea,
kujadili na kupitisha/kutopitisha maombi ya wanachama wapya.
- Kupokea
na kuufanyia kazi ushauri wa kitaalamu/kiufundi unaotolewa na wataalamu wa
kiufundi.
- Kufanya
maandalizi ya Mkutano Mkuu wa kawaida muda unapokaribia wa kufanyika na
Mkutano Mkuu maalumu/dharula unapohitajika.
- Kutathmini
mwenendo wa utendaji wa viongozi pamoja na wanakikundi kwa uwazi, ukweli
na haki.
- Kuandaa
na kuwasilisha mapendekezo ya maboresho/marekebisho ya Katiba kwenye
Mkutano Mkuu wa kawaida.
4.9.4 VIKAO VYA KAMATI
Vikao vya Kamati zote
vitafanyika mara moja kila mwezi na kwamba vikao vitakuwa vikifanya mapitio ya
mara kwa mara kuhusu utekelezaji wa Mipango na Shughuli za kikundi. Majukumu ya
kamati yatakuwa ni kama yalivyoainishwa kwenye kipengele 4.2 hapo juu.
4.10
TAARIFA ZA MIKUTANO NA VIKAO
- Mikutano
yote ni sharti itolewe taarifa ya kufanyika si pungufu ya siku kumi na nne
(14) kabla ya kufanyika na agenda zilizopendekezwa ni sharti zibainishwe
na mlango utakuwa wazi kwa siku saba (7) zaidi ili wenye agenda nyingine
tofauti na zilizopendekezwa waweze kuziwasilisha kwa Katibu Mtendaji kwa
uchambuzi na mapitio kabla ya kuingizwa kwenye ajenda za mikutano/vikao.
- Vikao
vya Kamati zote vinaweza kuitishwa kufanyika kulingana na mahitaji pasipo
kigezo cha kutoa taarifa rasmi katika kipindi fulani.
- Mihtasari
yote ya vikao na/au mikutano itaandaliwa na kusomwa kwenye mkutano au
kikao kinachofuata.
4.11 IDADI YA WAJUMBE
WANAOHALALISHA MKUTANO / KIKAO
Kikao au Mkutano wowote
utaweza kufanyika pale utakapokuwa na idadi ya wajumbe waliotarajiwa kuhudhuria
kufikia nusu (1/2) na kuendelea.
4.12 TARATIBU ZA UPIGAJI KURA KATIKA
CHAGUZI
- Katika uchaguzi wowote
utakaofanyika ni sharti kuwa, kura zote zitapigwa kwa siri.
- Kila
mjumbe atakuwa na haki ya kupiga kura moja kwa mgombea mmoja.
- Endapo
itatokea kura kulingana mara mbili mfululizo, basi Mwenyekiti ana haki ya
kutumia kura ya turufu ili mshindi aweze kupatikana.
- Ili
mgombea yoyote ikiwa pamoja na nafasi ya Mwenyekiti aweze kuchaguliwa na
kutangazwa mshindi basi ni sharti apate kura zaidi ya wagombea wengine
wote.
SEHEMU YA
TANO
MASUALA
YA KIFEDHA KATIKA KIKUNDI
5.1 VYANZO VYA MAPATO YA
KIKUNDI
Kwa mujibu wa Katiba hii
vyanzo vya mapato ya kikundi ni kama ifuatavyo:-
i. Viingilio
vya uanachama.
ii. Ada ya kila mwaka ya uanachama.
iii. Ruzuku mbalimbali.
iv. Miradi ya Uzalishaji mali.
v. Michango ya hiari toka kwa wanachana na wadau wengine.
vi. Misaada kutoka nje ya kikundi.
viii.
Mikopo kutoka taasisi za
kifedha.
Michango yo yote
itapokelewa na kukatiwa stakabadhi ili kuthibitisha na kukiri kupokea
mchango/michango hiyo.
5.2 KIINGILIO, ADA NA
MICHANGO MBALIMBALI
Kutakuwa na Kiingilio cha
Uanachama, Ada ya uanachama ya mwaka pamoja na michango mbalimbali ambayo
wanachama watakuwa wakihitajika kutoa baada ya kukubalika kupitia vikao halali
vya kikundi. Viwango vya michango hiyo vitakuwa kama ifuatavyo:-
i. Kiingilio cha Uanachama
Kiwango cha Kiingilio cha uanachama kwa mtu anayehitaji kujiunga na
kikundi binafsi kitakuwa ni Shilingi Elfu Thelathini za Kitanzania (TSZ. 30,000/=)
ii.
Ada ya Uanachama ya Mwezi
Kiwango cha ada ya mwezi kwa mwanachama kitakuwa ni shilingi elfu kumi
za kitanzania (TSZ. 10,000/=) tu.
ii.
Michango ya Hiari
Kutakuwa na michango ya hiari ambayo mtu hatolazimishwa bali anaweza
kujitolea mali au fedha kwa mapenzi yake mwenyewe na kwa lengo la kukijenga na
kukiendeleza kikundi.
SEHEMU YA SITA
USIMAMIZI WA MALI NA RASLIMALI
6.1 USIMAMIZI WA VIFAA
Mali na raslimali zote za
kikundi zitasimamiwa kwa kuhakikisha yanafanyika yafuatayo:-
i. Mali na raslimali zote zitaorodheshwa katika Regista
maalum.
ii. Mali zote na raslimali zitawekwa alama/namba ya utambulisho.
6.2 USIMAMIZI WA FEDHA
- Kutakuwa
na Akaunti za Akiba na Hundi katika Benki.
- Akaunti
za kikundi zitafunguliwa katika Benki kati ya CRDB ua Benki zilizopo
karibu na makao makuu ya kikundi.
- Watia
sahihi (Bank Signatories) katika akaunti zote watathibitishwa na
wanakikundi. Kutakuwa na makundi mawili ya watia sahihi:-
Kundi A.
Katibu Mtendaji
Mwenyekiti.
Kundi B
Mweka Hazina
Mjumbe mmoja wa kamati ambayo siyo ya fedha (KE)
- Wawili
kati yao wataruhusiwa kuchukua fedha kutoka akaunti yoyote iliyopo katika
Benki yoyote (mmoja kutoka kila kundi la A na B). Endapo
dharula itajitokeza watia sahihi wote wawili wa kundi B hawapo, basi watia sahihi wawili wa kundi A wanaweza kuchukua fedha na si
kinyume chake
- Matumizi
yoyote ya kikundi ni lazima yapitishwe na kikundi. Fedha hazitachukuliwa
benki bila kuidhinishwa kwenye kikao cha wanakikundi au kamati tendaji.
- Mwaka
wa fedha wa kikundi utaanzia kila mwezi Julai na kuishia Juni ya mwaka
unaofuata.
SEHEMU YA SABA
MASUALA MENGINEYO
7.1. MASUALA MUHIMU YA KISHERIA
Masuala mengine ya
kisheria na kanuni katika kikundi ni pamoja na:-
- Kikundi
kitaenendesha shughuli zake kwa lugha za Kiswahili.
- Kamati
tendaji ina haki ya kutoa mapendekezo ya kubadilisha viwango vya kiingilio
na ada pamoja na vipengele vya Katiba na kuwasilisha kwenye Mkutano Mkuu
kwa mjadala na maamuzi ya mwisho.
- Kikundi
kitakuwa tayari kupokea misaada, ruzuku na mikopo toka kwa wafadhili na/au
wahisani ikiwa tu misaada, ruzuku na mikopo hiyo inaendana na malengo na
masharti ya kikundi kwa mujibu wa Katiba hii.
- Jambo
lolote ambalo litaleta utata wa kitafsiri ndani na nje ya Katiba hii, basi
tafsiri sahihi itatolewa au kuamuliwa na wanakikundi wenyewe.
- Kikundi
kina haki ya kushitaki au kushitakiwa kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
7.2
MWAKA WA KIKUNDI
Mwaka wa kikundi utakuwa
kuanzia 01/01 hadi 31/12/
7.3 KUFA / KUSAMBARATIKA KWA
KIKUNDI
Kikundi cha WAKULU WA UKAYA
kipo kwa ajili ya kuwasaidia na kuwawezesha wanakikundi kujiendeleza kiuchumi. Kutokana na malengo yake inategemewa kuonekana kuwa kikundi ni endelevu.
Hata hivyo endapo kikundi kitasambaratika mali ya kikundi itawekwa chini ya
uangalizi wa serikali ya wilaya ambacho kikundi kipo. Serikali ngazi ya wilaya itasimamia
ugawanyaji wa mali kwa wanakikundi pale itakapobidi na kama kuna rasilimali
zilizotokana na wafadhili rasilimali hizo zitapewa taasisi nyingine inayofanya
kazi za maendeleo zinazofanana na kikundi hiki. Hata hivyo Serikali haitakuwa
na mamlaka ya kuingilia shughuli za kiutendaji za kikundi wakati wote wa uhai
wake isipokuwa itakapohitajiwa msaada wa kufanya hivyo.
KATIBA
HII IMEKUBALIWA NA KUPITISHWA RASMI NA
WANACHAMA
WAANZILISHI LEO TAREHE ……………………………….
No comments:
Post a Comment