HISTORIA, MILA NA DESTURI ZA WAKAGULU
Wakagulu ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Morogoro, Wilaya ya Kilosa. Lugha yao ni Kikagulu. wakagulu ni... mojawapo ya makabila makubwa katika mkoa wa Morogoro, wakagulu zaidi wapo katika wilaya za Kilosa, Gairo, Mpwapwa, Kongwa, Kiteto na sasa wanatanuka zaidi maeneo ya handeni. Ukifuatilia Simulizi za wazee, hususani wakati wa sherehe za kumaliza msiba (mwidiki) inaonesha kuwa wakagulu walitokea maeneo ya Rwanda na Burundi (ya sasa). Walitoka meaneo ayo kutokana na ukame uliokuwepo na matatizo mengine ya kivita. Walipita maeneo mengi yakiwemo KONONGO(UKIMBU)., Mkoani Rukwa baadaye walipita maeneo ya Mkoa wa Singida hadi wakaingia RUDI (KUSINI MWA MPWAPWA).Baada ya kuishi hapo kwa muda waliparamia milima ya Rubeho, lakini bado walikuwa na mawasiliano makubwa na watu wa Konongo. Katika kuzunguuka hapa na pale huko milimani ndipo zilipojitokeza Koo mbalimbali za wakagulu kutokana na matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiwapata wanawake. Kwa msingi huo wakagulu wanachukua ukoo ( welekwa )kutoka kwa mama. Kwa mfano ukoo wa Wambigo ulipatikana baada ya wahenga kukanyaga maji yaliyokuwa yanajizunguusha (Gakubiga) kwenye mto Mkondoa. Hao ndio Wakagulu.
NGOMA YA KIKAGULU AINA YA "ISUMBI"
Safi sana sisis kama Ago Media tunakwambia tumeiweka historia ya wakaguru soon itakuwa hewani tembelea youtube channel yetu ya Ago TV subscribe ilikuweza kupata uptade yetu
ReplyDeleteNawashukuru kwa kusema historia hiyo
ReplyDelete