ASILI YA WAKAGULU
Wakagulu ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa
wa Morogoro, Wilaya
ya Kilosa. Lugha yao ni Kikagulu... wakagulu ni mojawapo ya makabila makubwa katika mkoa wa Morogoro,
wakagulu zaidi wapo katika wilaya za Kilosa, Gairo, Mpwapwa, Kongwa, Kiteto na
sasa wanatanuka zaidi maeneo ya handeni. Ukifuatilia Simulizi za wazee,
hususani wakati wa sherehe za kumaliza msiba (mwidiki) inaonesha kuwa wakagulu
walitokea maeneo ya Rwanda na Burundi (ya sasa). Walitoka meaneo hayo kutokana
na ukame uliokuwepo na matatizo mengine ya kivita. Walipita maeneo mengi
yakiwemo KONONGO(UKIMBU)., Mkoani Rukwa baadae walipita maeneo ya Mkoa wa
Singida hadi wakaingia RUDI (KUSINI MWA MPWAPWA). Baada ya kuishi hapo kwa muda
waliparamia milima ya Rubeho, lakini bado walikuwa na mawasiliano makubwa na
watu wa Konongo. Katika kuzunguuka hapa na pale huko milimani ndipo
zilipojitokeza Koo mbalimbali za wakagulu kutokana na matukio mbalimbali
yaliyokuwa yakiwapata wanawake. Kwa msingi huo wakagulu wanachukua ukoo (
welekwa )kutoka kwa mama. Kwa mfano ukoo wa Wambigo ulipatikana baada ya
wahenga kukanyaga maji yaliyokuwa yanajizunguusha (Gakubiga) kwenye mto
Mkondoa.
No comments:
Post a Comment